Amri ya Rais wa Marekani, Donald Trump ya kuwazuia wahamiaji, wageni na wakimbizi kutoka nchi 7 za kiislamu kuingia Marekani imetenguliwa na mahakama, hivyo wahamiaji wote na wakimbizi wote wanaruhusiwa kuingia Marekani mpaka hapo kesi itakaposikilizwa mwezi wa pili..
Jaji wa Seattle ameeleza kutokubaliana na sababu zilizotolewa na mawakili wa Serikali na kusema kuwa amri hiyo inaweza kusimamishwa mara moja huku kesi hiyo ikiendelea kusikilizwa mahakamani.
Kufuatia amri hiyo ya mahakama, wahamiaji na wageni wa nchi hizo waliozuiliwa wameachiliwa huru na wameweza kuingia Marekani.
Hata hivyo, Serikali inatarajiwa kukata rufaa ya dharura dhidi ya uamuzi huo wa mahakama, ambao ni changa moto kubwa kwa utawala wa Trump.
Serikali ya Marekani inasema kuwa visa nyingi zimefutiliwa mbali tangu rais Trump kutia sahihi amri ya kupunguza idadi ya watu wanaopaswa kuingia nchini Marekani juma lililopita.