Mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali ameachiwa huru baada ya Mahakama Kuu kanda ya Dar es salaam kutengua hukumu ya kifungo cha miezi sita gerezani iliyotolewa na Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Kilombero, Morogoro.
Mahakama Kuu Dar es salaam imetengua hukumu hiyo leo Machi 30, 2017 baada ya kukuta Mbunge huyo hana kosa na hivyo kutengua hukumu hiyo.
Mbunge Lijualikali awali alihukumiwa kifungo cha miezi sita baada ya kukutwa na kosa la kufanya fujo na kusababisha taharuki wakati wa uchaguzi wa Mwenyekiti na makamu wake wa Halmashauri ya Kilombero.