Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam leo August 4, 2017 imetupilia mbali pingamizi la Wabunge 8 wa  Viti Maalumu waliofutwa uanachama na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Prof. Ibrahim Lipumba ya kutaka wabunge 8 walioteliwa wasiapishwe na Bunge.

Amuzi hilo limetolewa leo kufuatiwa kesi iliyofunguliwa na Wabunge 8 waliofutiwa uanachama na kuiomba mahakama kuu itoe amri ya zuio kwa wabunge walioteuliwa kutoapishwa mpaka kesi yao itaposikilizwa na kutolewa maamuzi.

Leo Jaji Lugano Mwandambo amesema ametupilia mbali pingamizi hilo lililozuia Wabunge hao 8 kuapishwa.

Jaji Lugamo ameeleza sababu ya kufutilia mbali shitaka hilo na kusema katika sheria hakuna kifungu maalumu kinachoeleza maombi hayo yasiwe sahihi na kuzuia wabunge hao wasiapishwe.

Kupitia taarifa hiyo ya kufutilia mbali pingamizi la uapisho wa wabunge hao, wabunge wapya walioteuliwa kuziba nafasi wanaweza kuapishwa wakati wowote kuanzia sasa.

Wabunge waliovuliwa ubunge ni Pamoja na Miza Bakari, Saverina Silvanus Mwijage, Salma Mohamed Mwassa, Raisa Abdallah Mussa, Riziki Shairi Mngwali, Hadija Salumu, Halima Ali Mohammed na Saumu Heri Sakala.

 

 

 

 

Dr. Kingwangalla awachachua wafuasi wake Twitter
Siku zake zahesabika, amtendea mkewe unyama mbele ya watoto wao