Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu imetoa hati ya kumkamata msanii wa filamu nchini, Wema Sepetu kwa kosa la kukiuka masharti ya dhamana baada ya upande wa mashtaka kudai kwamba mshtakiwa hayupo mahakamani na hakuna taarifa yoyote.

Wakili wa utetezi wa msanii huyo, Ruben Simwanza amedai kuwa mshtakiwa alifika Mahakamani lakini aliumwa hivyo alishindwa kuingia katika chumba cha mahakama.

Akitoa uamuzi huo Hakimu Maira amesema Mahakama inatoa hati ya kumkamata kwa sababu kama alifika alishindwa nini kuingia ndani.

Msanii huyo anadaiwa kusambaza video zenye maudhui ya ngono kupitia ukurasa wake wa Instagram Oktoba 15, mwaka jana.

TTCL, TANESCO waongoza kwa deni kubwa pango la ardhi
Kampuni ya simu ya TECNO yatoa Ofa kwa wateja wake

Comments

comments