Mahakama ya Kisutu jijini dar es salaam imemsomea mashtaka yanayomkabili mwanadada Agness Gerald maarufu kama ‘Masogange’ ambaye ni ‘Video Queen’ anayeonekana kwenye video mbali mbali za muziki wa Bongofleva leo baada ya ufikishwa Mahakamani hapo.

Hata hivyo mara baada ya kusomewa mashtaka hayo mahakamani hapo mtuhumiwa alikana mashtaka, na ndipo Mahakama ikatoa masharti ya dhamana na mtuhumiwa kufanikiwa kuyatimiza.

Masogange yupo nje kwa dhamana ya shilingi Milioni 10 na hatakiwi kusafiri nje ya Dar es salaam na hadi itakapo sikilizwa tena March 22, 2017.

Masogange ameshikiliwa kwa siku kadhaa na jeshi la Polisi kwa tuhuma za kujihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya.

Wachina Kuinunua AC Milan
Ridhiwani: Sifanyi biashara haramu, ni bora kufa maskini kuliko kutafuta utajiri kwa njia hiyo.