Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa ameridhia uamuzi wa Mahakama ya Katiba uliothibitisha ushindi wake kufuatia uchaguzi mkuu, baada ya majaji kutupilia mbali madai ya upinzani yakitaka matokeo ya uchaguzi huo yafutwe kwa madai ya kuwa kulikuwa na wizi wa kura.
Mahakama Kuu imetupilia mbali ombi la upinzani wakitaka matokeo ya uchaguzi yabatilishwe kwa tuhuma za kuwa uchaguzi ulichakachuliwa na kumpa ushindi mrithi wa Robert Mugabe, Emmerson Mnangagwa
“Mara nyingine tena nasisitiza wito wangu wa kuimarisha amani na umoja kuliko suala lolote jingine, Sote hivi sasa tuweke pembeni tofauti zetu. ni wakati wa kusonga mbele kwa kushirikiana kwa pamoja.”ameandika Mnangagwa katika ukurasa wake wa Twitter
Aidha, katika uchambuzi wake wa mwisho, mahakama hiyo imegundua kuwa upinzani wameshindwa kupeleka ushahidi uliowazi na unaojitoshereza.
-
Mnangagwa alivyoishawishi Mahakama kutokubali ya Chamisa
-
Kesi ya Uchaguzi Zimbabwe: Wapinzani wataja ulawiti kwa mawakala
-
Congo DRC yawakataa wasimamizi wa uchaguzi wa Kimataifa
Hata hivyo, Wachambuzi wa mambo ya kisiasa walikuwa wametabiri kwa upana kuwa mahakama itafanya uamuzi dhidi ya kesi iliyofunguliwa na chama cha upinzani cha Democratic Change Party kupinga matokeo.