Mahakama Jijini kigali nchini Rwanda imewaachia huru mwanasiasa wa upinzani, Diane Rwigara na mama yake Adeline Rwigara na kutangaza kuwa hawana hatia na kwamba mashtaka dhidi yao hayana msingi wowote.
Mahakama imesema kuwa imechukua uamuzi huo kutokana na kwamba upande wa mashitaka haukutoa ushahidi wa kutosha.
Wawili hao walishitakiwa kwa makosa ya kuchochea vurugu na mgawanyiko miongoni mwa wananchi pamoja na kughushi nyaraka.
Kwa upande wa muendesha mashtaka alikuwa ameiomba mahakama kuwapa kifungo cha miaka 22 jela kutokana na tuhuma zilizokuwa zikiwakabili.
Aidha, uamuzi huo ulikuwa ukisubiliwa kwa hamu na wafuasi wake baada ya Diane Rwigara na mama yake Adeline Mukangemanyi kukamilisha kesi hiyo wakiwa hawako kizuizini.
-
‘Marufuku daladala kuingia katikati ya jiji, watu wafanye mazoezi’
-
Mahakama Kuu yapiga chini marufuku ya Serikali kuhusu daladala
-
Hatma ya Diane Rwigara na familia yake kufahamika
Hata hivyo, kwa mshangao wa wengi , mapema mwezi wa 10 mwaka huu mahakama ilichukua uamuzi wa kuwaachilia huru kwa dhamana ikisema sababu za kimsingi zilizosababisha kesi yao kusikilizwa wakiwa kizuizini hazipo tena.