Mahakama Kuu ya Tanzania kitengo cha ardhi jana alitoa hukumu ya kesi ndogo (awali) na kuweka zuio la kubomoa nyumba takribani 681 za wakazi wa Kinondoni hadi kesi ya msingi itakaposikilizwa.

Jaji wa mahakama hiyo, Panterine Kete alieleza kuwa uamuzi huo umetolewa baada ya mahakama kusikiliza maelezo ya pande zote mbili na kuangalia madhara watakayoyapata wananchi waliofungua kesi hiyo kufuatia zoezi la bomoabomoa.

Hata hivyo, Jaji Kete alisisitiza kuwa zuio hilo ni kwa nyumba za wananchi waliofungua kesi mahakamani na sio kwa nchi nzima. Aliongeza kuwa serikali itaendelea kuweka alama za X kwa nyumba ambazo zimejengwa katika maeneo hatarishi.

Kesi ya msingi iliyofunguliwa mahakamani hapo na mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia na wananchi nane wakiwakilisha wananchi wengine wa eneo hilo kupinga zoezi la Bomoabomoa hadi wananchi wote watakapopewa stahiki zao ikiwa ni pamoja na viwanja, imepangawa kusikilizwa Januari 11 mwaka huu.

Zoezi la bomoabomoa liliendelea jana ambapo takribani nyumba 100 zilivunjwa katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam.

Picha: Mwanamke mrembo achinjwa kwa kuipinga ISIS
Zitto Aishangaa serikali kulilea jipu hili