Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama amesema kuwa wameanzisha rasmi zoezi la ukamataji maharamia wa kazi za wasanii  amabo ni wauzaji wa filamu feki, ambapo zoezi hilo linatrajiwa kufanyika Tanzania nzima.

Kwa sasa zoezi hilo limekwishafanyika mkoa wa Dar es salaam na zaidi ya maharamia 200 wauzaji wa filamu feki za wasanii wamekamatwa  na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mapema wiki ijayo.

Msama anaishukuru Serikali ya awamu ya tano ya Magufuli kwa suhirikiano ambao wamekuwa wakiuonesha katika kukomesha tabia ya wamachinga kuuza filamu zisizo na stika kutoka TRA.

‘’Ndugu zangu waandishi nimewaita hapa kuwaeleza juu ya zoezi la kuwakamata maharamia wa kazi za sanaa bado linaloenedelea vizuri na sasa wanatarajiwa kufikishwa mahakamani wiki ijayo ili waweze kusomewa mashtaka yao’’. amesema Msama.

Msama amesema kuwa mpaka sasa msako huo umefanikisha kukamata vifaa vya zaidi ya bilioni 1 ikiwemo kompyuta na cd feki.

Ameongeza kuwa kuwa Watanzania lazima walipe kodi na wauze kazi zilizo na stika ili kuliongezea taifa mapato.

Hata hivyo zoezi la ukamataji wa kazi feki litaendelea katika mkoa  wa Morogoro, ikiwa ni zoezi la nchi nzima.

Breaking News: Anna Mghwira atangaza kujiunga CCM
Mwalimu amkung'uta makonde Mwalimu Mkuu