Maharamia wameripotiwa kuvamia meli ya mizigo ya Uswizi na kuteka wahudumu 12 wa meli katika bahari ya eneo la Nigeria.

Mamlaka zimeeeleza kuwa maharamia hao waliivamia MV Glarus siku ya Jumamosi, wakati meli hiyo ikifanya safari yake kutoka Lniagos kwenda bandari ya Harcourt.

Kwa mujibu wa AFP, maharamia hao walitokea mbali, waliharibu vifaa vya mawasiliano vya meli hiyo pamoja na kukata waya muhimu za uendeshaji.

Kampuni ya Massoel Shipping, imeleza kuwa maharamia hao walitokea eneo la kisiwa cha Bonny kilichoko eneo la Niger Delta, nchini Nigeria.

Msemaji wa kampuni ya Massoel amesema kuwa familia za wahudumu waliotekwa zimekuwa zikipewa taarifa ya ndugu zao na hali ilivyo kwa ukaribu.

Waziri wa mambo ya nje wa Uswizi amesema kuwa kati ya waliotekwa hakuna aliyekuwa raia wa nchi hiyo, wengi wakiwa wanatoka Ufilipino, Romania, Ukraine, Croatia na Slovenia.

NB: Picha sio ya tukio hili

Nape Nnauye apata ajali mkoani Lindi
Video: Lissu ataka Majaliwa, Kamwelwe wang'oke, JPM atumbua vigogo sita