Ni mojawapo ya maeneo machache duniani ambapo watu wanaweza kukutana na kuingia kwenye Bwawa la kuogelea lililojaa pombe maalum, linalopatikana katika Jumba la kifahari la Starkenberger’s la kampuni ya bia ya Austria inayotoa uzoefu kamili unaozingatia matumizi wanayodai kuwa ni ya kiafya.

Bwawa hili linapatikana katika kasri hilo na linadaiwa kuwa ni la kipekee na maalum kwa kuogelea bia Duniani likiwa na madimbwi saba ya bia joto ya urefu wa futi 13 na kila moja ikiwa na pinti 42,000 ambapo mtu anaweza kuketi na kuoga na kupumzika kabisa.

Inadaiwa kuwa Bia hiyo ina vitamini na kalsiamu nyingi, na inasemekana ukiogelea ni nzuri kwa ngozi yako na husaidia kuponya majeraha ya mbalimbali mwilini ya nje na ndani.

Mabwawa hayo, yalianza kutumika rasmi mwaka 2005 wakati pishi la zamani la kuchachusha pombe la ngome ya miaka 700 lilipopitwa na wakati, kwa hivyo waligeuza eneo hilo kuwa la kuhifadhia bia na hairuhusiwi kunywa Bia iliyopo katika bwawa la kuogelea.

David de Gea awindwa Ujerumani
MSD kuongeza kasi usambazaji bidhaa za Dawa