Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya – DCEA, Aretas Lyimo amewataka Vijana kuacha matumizi ya Dawa za kulevya ikiwemo uvutaji bangi kwa imani kuwa watarahisisha maisha au kusoma zaidi.

Lyimo ameyasema hayo hivi karibuni wakati alipokuwa akiongea na Dar24 Media jijini Dar es Salaam kuhusu zoezi la utoaji wa elimu kwa jamii juu ya sheria zinazoongoza Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, madhara na aina ya Dawa za kulevya.

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya – DCEA, Aretas Lyimo.

Amesema, “Wanafunzi ndio kundi kubwa linaloathirika na Dawa za kulevya wengi wanaingia kwa kutokujua wakiamini kuwa wakivuta au wakivuta Dawa za kulevya au wakivuta bangi basi watasoma zaidi, watakuwa na akili sana, watamudu masomo yao au kurahisisha maisha lakini mwisho wa siku wanaanguka vibaya.”

Aidha, Kamishna Jenerali ameongeza kuwa hatua hiyo imewafanya DCEA kujikita katika utoaji wa elimu maeneo mbalimbali ikiwemo yale wanayofanya operesheni ya Dawa za kulevya akisema, “baada ya kukamata watu pia tunatoa elimu kwenye jamii ili wasiendelee kujiingiza katika jambo hilo.”

Twaha Kiduku atamba kumchakaza Godi Apei
Dkt. Mwinyi akemea urasimu kwenye biashara