Kiungo mshambuliaji wa mabingwa wa soka nchini Hispania FC Barcelona Arda Turan, huenda akaondoka Camp Nou na kutimkia mshariki ya mbali (China).
Wakala wa kiungo huyo Ahmet Bulut, aliwasili mjini Barcelona mwishoni mwa juma lililopita kwa ajili ya kuitikia wito wa mchezaji wake ambaye amekua hachezi mara kwa mara katika kikosi cha kwanza cha FC Barcelona.
Baadhi ya vyombo vya habari mjini Barcelona vimeeleza kuwa, wakala wa Turan amekua na mahusiano mazuri na baadhi ya klabu za soka nchini China.
Hata hivyo tetesi zinaeleza kuwa, klabu ya Guangzhou Evergrande imejipanga kumsajili Turan kwa ada ya uhamisho wa Euro milioni 50 huku ikimtengea mshahara wa Euro milioni 20 kwa mwaka.
Turan aliwahi kukataa ofa ya klabu hiyo mwishoni mwa mwaka jana, lakini hisia za kutaka kuihama FC Barcelona zinaonekana kuibuka tena na kufikia hatua ya kufanya mazungumzo na wakala wake.