Jaji Mkuu, Othman Chande amesema kuwa Tume ya Mahakama imekamilisha uchunguzi wa awali kuhusu majaji wanaotuhumiwa katika sakata la Escrow kwa kupokea mgao wa fedha kutoka kwa Mkurugenzi wa VIP engineering, James Rugemalira.

Jaji Othmani Chade amesema hayo jana Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya Rais Jakaya Kikwete kuwaapisha majaji 14, kati yao mmoja akiwa jaji wa mahakama ya rufaa, Richard Mzirai. Na wengine 13 wakiwa wa Mahakama Kuu.

Alieleza kuwa mahakama itakaa kupitia ripoti ya uchunguzi huo na kutoa mapendekezo yao kwa mamlaka za uteuzi.

Majaji wanaouhusishwa na sakata hilo la Escrow ni pamoja na Profesa Eudes Ruhangisa anayetuhumiwa kupokea zaidi ya shilingi milioni 404 za Rugemalira na Jaji Aloyce Mujulizi aliyepewa shilingi milioni 40.4.

Sakata la Escrow liliwatia doa watu mbalimbali wenye nyadhifa kubwa za chama na serikali na kupelekea waziri wa Nishati Na Madini, Sospeter Muhongo na aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kujiuzulu nyadhifa zao.

Anna Tibaijuka na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge ni moja kati ya viongozi wanaofikishwa mbele ya tume ya Maadili kufuatia sakata hilo.

Kagame Cup 2015 Yaongeza Neema Azam FC
Sturridge Uso Kwa Uso Na Man Utd Septemba 12