Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemuagiza Kamanda wa TAKUKURU wa wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Francis Zuakuu kumkamata aliyekuwa Mtendaji wa Kijiji cha Bulagamilwa, Ntemi James kwa tuhuma za kuhusika na upotevu wa sh. milioni 141 za kijiji hicho.

Ametoa agizo hilo wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Igunga, akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani Tabora.

Aidha, amefikia uamuzi huo mara baada ya Mbunge wa Manonga, Seif Gulamali kumuomba awasaidie katika kulipatia ufumbuzi suala hilo la upotevu wa fedha za kijiji kwa kuwa ni la muda mrefu na hakuna hatua zilizochukuliwa.

“Msimamo wa Serikali ni kuhakikisha wananchi wanahudumiwa ipasavyo, hivyo haitawavumilia watumishi watakao jihusisha navitendo vya rushwa na matumizi mbaya ya fedha za umma.”amesema Majaliwa

Hata hivyo, Majaliwa amewataka wakuu wa idara na watumishi wengine wajiwekee utaratibu wa kuwatembelea wananchi katika maeneo yao hususan ya vijijini kwa ajili ya kusikiliza kero zinazowakabili na kushirikiana nao katika kuzipatia ufumbuzi.

Video: Waziri Mkuu aagiza Mtendaji akamatwe, "Leo nalala hapa, hadi saa moja nipate majibu"
Ospina asitisha usajili wa Mignolet SSC Napoli