Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameagiza watumishi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyangw’ale waliohusika na ubadhilifu wa zaidi ya sh. bilioni tatu fedha ambazo zilitolewa na Serikali kugharamia miradi ya maendeleo wachukuliwe hatua.
 
Pia ameagiza kukamatwa na kuchukuliwa hatua kwa Mkaguzi wa Ndani wa halmashauri hiyo, Gavana Matesa kwa sababu ameshindwa kutoa kwa mamlaka husika kuhusu taarifa za wizi wa fedha za maendeleo zilizotafunwa.
 
Ametoa agizo hilo wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Nyangw’ale akiwa katika ziara yake ya kikazi ya siku nne mkoani Geita.
 
Aidha, miongoni mwa miradi ambayo fedha zake zimepotea ni pamoja na sh. bilioni 1.2 za ujenzi ofisi ya halmashauri hiyo, sh. milioni 400 za ukarabati wa kituo cha afya Nyangw’ale, sh. milioni 611.230 za miradi ya maji.
 
Nyingine ni sh. milioni 536.119 za mpango wa malipo kulingana na huduma (EP4R), sh. milioni 125.914 za ushuru wa huduma, sh. milioni 31 za ujenzi wa ofisi ya mbunge na sh. milioni 109 za mfuko wa barabara.
 
“Wilaya ya Nyangw’ale ni mpya na Serikali imekuwa ikileta fedha nyingi lakini fedha zote zimetafunwa, Serikali ipo makini sana na moja kati ya vita kubwa ni dhidi ya mafisadi, wala rushwa ambayo ni endelevu hivyo tutashughulika na kila mmoja,”amesema Majaliwa
 
  • Watumishi watakiwa kuongeza ubunifu
 
  • Mhadhiri alia na rushwa ya Ngono UDSM, amtaka JPM kuingilia kati
 
  • Vyama vya upinzani vyaungana kuhusu kesi ya Mbowe na Matiko
 
Hata hivyo, mpaka sasa watu saba akiwemo aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Nyangw’ale, Carlos Gwamagobe na wenzake wamekamatwa

Anachofanya Makonda ni uchonganishi- Saed Kubenea
Vyama vya upinzani vyaungana kuhusu kesi ya Mbowe na Matiko