Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali kupitia Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama ndoo kichwani, itahakikisha wananchi katika maeneo yote nchini wanapata huduma ya maji safi na salama karibu na maeneo yao ya makazi.
Ameyasema hayo alipozungumza na wananchi kwenye kijiji cha Nyamirembe baada ya kukagua na kuweka jiwe la msingi katika mradi huo wa maji wakati akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake mkoani Geita.
Amesema kuwa Serikali imedhamiria kuhakikisha wananchi wote nchini wakiwemo wa wilaya ya Chato mkoani Geita wanapata huduma ya maji safi na salama karibu na makazi yao, hivyo amewataka waendelee kuwa na imaji na Serikali yao.
“Serikali ya Awamu ya Tano ina mikakati mizuri inayolenga kumaliza tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwenye maeneo mbalimbali nchini vikiwemo na vijiji vya wilaya ya Chato ili kuwawezesha wananchi kupata maji.”amesema Majaliwa
Aidha, Majaliwa ameagiza mradi huo ukamilike kwa wakati kwa kuwa Serikali inahitaji kuona wananchi wakinufaika na huduma hiyo. Mradi huo ulianza kujengwa Mei, 2017 na ulitakiwa ukamilike Mei, 2018 ila kutokana na changamoto mbalimbali unatarajiwa kukamilika Februari 2019.
-
RC Mndeme afuta likizo za watumishi
-
JPM amng’ata sikio Lowassa kuhusu Wapinzani
-
BREAKING NEWS: Rais Magufuli akihutubia katika uzinduzi wa Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam
Kwa upande wake, mkuu wa wilaya ya Chato Mhandisi, Mtemi Simeon amesema kuwa mradi huo unatarajiwa kuhudumia watu takribani 59,609 katika vijiji 11 vilivyopo kwenye kata nne za Nyamirembe, Ichwankima, Kachwamba na Kasenga, ambapo amevitaja vijiji hivyo kuwa ni Nyamirembe, Kalebezo, Nyambiti, Busalala, Imalabupina, Ichwankima, Kachwamba, Ipandikilo, Idoselo, Igagula na Mwangaza.