Jeshi la Polisi mkoani Tabora limeagizwa kuwakamata viongozi wanne wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Tumbaku (WETCU) pamoja na kufunga ofisi za chama hicho kufuatia tuhuma za ubadhirifu wa fedha za chama hicho zinazowakabili.

Agizo hilo limetolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Machi 16, 2017 katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Isike Mwanakiyungi mkoani Tabora, ambapo amesema Rais Dkt. John Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa TTB, Vita Kawawa pamoja na Mtendaji Mkuu wa Bodi hiyo, Wilfred Mushi

Mwenyekiti wa WETCU, Gabriel Mukandara (katikati) na Makamu wake, Msafiri Ngassa wakiongozwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Hamis Issah (kulia) kuelekea kwenye gari la polisi baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuagiza kuwa wakamatwe na kuwekwa ndani hadi uchunguzi kuhusu utendaji wao utakapokamilika. Majaliwa alikuwa akizungumza na Wadau wa zao la tumbaku kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Machi 16, 2017.

Majaliwa amemwagiza Kamanda wa Polisi kuwakamata viongozi hao hadi uchunguzi wa tuhuma hizo utakapokamilika, ambapo pia amevunja Bodi ya WETCU pamoja na  Bodi ya Tumbaku Tanzania  – TTB kwa sababu ya kushindwa kusimamia zao hilo pamoja na matumizi mabaya ya fedha za umma.

Viongozi wanaotakiwa kukamatwa ni Mwenyekiti, Mkandara Mkandara, Makamu Mwenyekiti, Msafiri Kassim, Mkaguzi wa Ndani na Mhasibu Mkuu. Pia amewasimamisha kazi watumishi wa kitengo cha uhasibu wa chama hicho hadi uchunguzi utakapokamilika.

Mwenyekiti wa WETCU, Gabriel Mukandara na Makamu wake, Msafiri Ngassa (kushoto) wakiwa kwenye gari la polisi baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuagiza kuwa wakamatwe na kuwekwa ndani hadi uchunguzi kuhusu utendaji wao utakapokamilika. Majaliwa alikuwa akizungumza na Wadau wa zao la tumbaku kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Machi 16, 2017.

“Kuanzia sasa watumishi wote wa kitengo cha uhasibu pamoja menejimenti nimewasimamisha kazi pamoja na Mrajisi wa mkoa wa Tabora Deogratius Rugangila. Kamanda hakikisha ofisi hazifunguliwi kuanzia sasa hadi hapo timu ya ukaguzi  itakapokamilisha kazi yake,” amesisitiza.

Majaliwa amesema kuwa haiwezekani kuwa na ushirika ambao hauwasaidii wanachama. “WETCU walipokea sh. bilioni 15 ambazo walizikatia risiti na hazijaonekana. Pia waliwalipa wazabuni sh, bilioni 10 ambazo hawajazikatia risiti,” amesema Majaliwa.

Amesema kuwa chama hicho kimesababisha kupungua kwa uzalishaji kwa kiasi kikubwa kutokana na kuwa na menejimemti mbovu jambo ambalo limechangia wakulima wa tumbaku kukosa tija.

Aidha, Majaliwa amepiga marufuku ununuzi wa mbolea kutoka nje ya nchi wkatiikiwa inazalishwa hap nchini. Aidha, alimepiga marufuku matumizi ya kwa dola katika sekta ya tumbaku na badala yake zitumike fedha ya Kitanzania kwa sababu kitendo hicho kimekuwa kiwanyonya wakulima.

 

Magazeti ya Tanzania leo Machi 17, 2017
Jinsi familia zinavyoathiriwa na teknolojia