Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa leo amefanya ziara ya ukaguzi wa mahindi katika maghala ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) , Chang’ombe jijini Dar es salaam
Aidha, Majaliwa amefanya ziara hiyo ya ukaguzi wa maghala hayo ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea sehemu mbalimbali za jiji la Dar es salaam. Hata hivyo katika ziara hiyo ya ukaguzi wa Maghala, Majaliwa amekutana na uongozi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula (NFRA), wakiongozwa na Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula, Deusdedit Mpazi.