Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Jabir Shekimweri afanye uchunguzi kuhusu matumizi ya sh. milioni 70 zinazotolewa kila mwezi na Serikali kwa ajili ya kununulia dawa kwenye wilaya hiyo.

Ametoa agizo hilo wakati akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa shule msingi Mpwapwa, ambapo amepokea malalamiko ya wananchi juu ya ukosefu wa dawa. Dawa pekee wanazopewa ni za kutuliza maumivu tu.

“Kilichokuwa kinasemwa na wabunge bungeni nilidhani sicho, nikasema nakuja niyasikie mwenyewe. Kweli wananchi hawaridhiki nimeona. Sasa mkuu wa wilaya shughulikia hili jambo ili kubaini fedha za dawa zinakwenda wapi.”amesema Majaliwa

Aidha, Majaliwa amesema kuwa lengo la Serikali kutoa fedha hizo kila mwezi ni kuhakikisha kwamba wananchi wote wanapata huduma za afya popote walipo badala ya kusafiri umbali mrefu kwenda makao makuu ya wilaya.

Hata hivyo, waziri mkuu amebainisha kuwa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imedhamiria kuwatumikia wananchi ipasavyo ikiwa ni pamoja na kuwapatia mahitaji muhimu kama huduma bora za afya na ndiyo sababu ya kutoa fedha hizo za dawa.

 

 

RC Wangabo awatahadharisha Wakurugenzi na Madiwani
Nick minaj, Card B waparamiana tena kisa 'like'