Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amenusa harufu ya ufisadi katika mradi wa ujenzi wa uzio wa makaburi ya Kola.

Eeneo ambalo wamezikwa watu 104 waliofariki dunia kutokana na ajali ya kupinduka na kulipuka kwa roli la mafuta eneo la Msamvu mkoani Morogoro.

Majaliwa amenusa ufisadi huo baada ya kubaini kuwa kimetengwa kiwango kikubwa cha fedha za ujenzi, hivyo amemuagiza Mkuu wa Mkoa huo, Dk. Stephen Kebwe, kusimamisha ujenzi hadi pale watakapo punguza gharama za ujenzi huo kutoka sh. milioni 30 za sasa hadi kufikia chini ya sh. milioni 10.

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo juzi, kwenye mkutano wake na wananchi wa Tarafa ya Mvuha, halmashauri ya wilaya ya Morogoro wakati akuhitimisha ziara yake ya siku tano mkoani humo.

” Nimeona hilo wakati nasomewa taarifa kuhusu ujenzi wa uzio kwa wenzetu walio tutangulia mbele ya haki kwa ajali ya moto nimesitisha huo ujenzi…, kujenga ukuta wa makaburi wala hakuhitaji kufunika kama uwanja wa mpira” alisema Majaliwa.

Aidha alitolea mfano wa ukuta uliojengwa kuzunguka makaburi ambayo wamezikwa watu waliokufa kwa ajali ya kuzama kwa kivuko, Ukerewe gharama zake hazikufika kama zilizowekwa katika makaburi hayo ya Kola.

Tanzania yapanda kwenye viwango vya FIFA
Misri yapata kocha mpya