Mkutano wa 10 wa Baraza la Mawaziri wa maji  Afrika (AMCOW) umefunguliwa jana na Waziri Mkuu wa Tanzania, Majaliwa Kasimu katika ukumbi wa Julius  Nyerere Dar es salaam huku akiwataka kuhakikisha changamoto za maji katika nchi za Afrika zinakwisha.

Waziri Mkuu, Majaliwa amewataka wataalamu wa masuala ya maji kutatua changamoto za upatikanaji wa maji safi na salama hasa vijijini kwa sababu nchi zake bado hazijamudu kuunganisha huduma hiyo katika maeneo hayo.

Majaliwa amewataka watafute njia sahihi itakayowezesha kutatua tatizo hilo kwa kutumia vyanzo mbalimbali vya maji vilivyoko huku http://bambawefushia.com/gratis-norsk/ mkutano huo ukiwa  unaokwenda sambamba na maadhimisho ya Wiki ya Maji Afrika.

”Tunategemea baada ya kumalizika kwa mkutano huu wataalamu wetu wataondoka na maazimio mazuri ya kumaliza tatizo la maji katika Bara letu kwa kutumia mito na maziwa ili kufikisha maji kwa wananchi.”-Majaliwa.

Akizungumzia kwa upande wa Tanzania alisema,  suala la maji limepewa kipaumbele hata katika bajeti ya mwaka huu na kwamba Serikali itahakikisha maji yanapatikana katika maeneo yote ili kutimiza sera yake ya kila mwananchi kupata maji umbali usiozidi mita 400.

Aidha Rais Mstaafu wa Kenya Mwai Kibaki ambaye ni Mjumbe Maalumu wa UNESCO kwa ajili ya masuala ya maji Barani Afrika alielezea umuhimu wa maji kwa maendeleo ya uchumi, hivyo wataalamu wanatakiwa kuhakikisha huduma hiyo inapatika katika maeneo yote.

Mkutano huo  wa siku tano unahudhuriwa Mawaziri wa Maji kutoka nchi 45 za Afrika na unaongozwa na Waziri wa Maji na Mazingira wa Senegal Amadou Mansour Faye ambaye ni Rais wa AMCOW.

Mario Gotze Kurejeshwa Westfalenstadion
Wakazi awaweka mkao wa kula mashabiki kuipokea Album yake