Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema kuwa vyombo vya dola vinatakiwa kupewa muda kwaajili ya kufanya uchunguzi katika matukio mbalimbali ya mashambulizi dhidi ya wananchi na viongozi.

Ameyasema hayo hii leo Bungeni Mjini Dodoma, wakati wa maswali na majibu mara baada ya kuulizwa swali na kiongozi wa kambi rasmi bungeni, Freeman Mbowe kuhusu kurusu vyombo vya kimataifa kufanya uchunguzi wa tukio la kushambuliwa kwa mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu

“Suala hili la kushambuliwa kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ni muendelezo wa matukio ambayo yamekuwa yakitokea sehemu mbalimbali nchini, ikiwemo mkoa wa Pwani katika Wilaya za Mkuranga, Rufiji na Kibiti, hivyo, vyombo vya dola vipewe muda wa uchunguzi ili kuwabaini waharifu,”amesema Majaliwa

Hata hivyo, ameongeza kuwa Tundu Lissu ni mbunge mwenzao hivyo suala hilo linamhusu kila mbunge wa kutoka upande wowote, hivyo linashughulikiwa kama matukio mengine yanavyoshughulikiwa.

 

Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Zimbabwe akimbia, Mke wa Mugabe atajwa kumrithi
Video: Bomu mkono lilivyoua wanafunzi..., Kashfa nzito vigogo sukari