Wakuu wa Mikoa, Wilaya kwa kushirikiana na wakurugenzi wameagizwa kusimamia kwa uzito unaostahili kampeni ya kuhamasisha Upimaji wa VVU itakayoendeshwa kwa muda wa miezi sita mfululizo.
Agizo hilo limetolewa Jijini Dodoma na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, ambapo amewataka viongozi kuhamasisha wananchi hasa wanaume kupima VVU na kama wakigundulika wameathirika basi waanze kutumia dawa mapema.
“Kwa vile tunazindua kampeni ya kupima na kuanza ARV mara moja (Test and Treat) natoa rai kwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na OR-TAMISEMI, mhakikishe vitendanishi na dawa za ARV zipo za kutosheleza katika kila kituo kinachotoa huduma katika kila Mkoa na Wilaya,” amesema Majaliwa.
-
Video: Mkuchika awakingia kifua watumishi waliotumbuliwa na wakuu wa mkoa, wilaya
-
JPM amteua Jaji Lubuva
-
Serikali yapigilia msumari wa moto wanaokamatwa Serengeti
Aidha, Majaliwa ametumia fursa hiyo kuwahamasisha watu wote watakaogundulika na maambukizo ya VVU waelewe kuwa utaratibu wa sasa ni kuanza dawa mara moja pasipo kujali kiwango cha kinga mwilini yaani CD4.
Hata hivyo, ameongeza kuwa huo ni utaratibu ambao nchi imeuridhia kwa kuwa una manufaa kwa mtumiaji wa dawa na jamii kwa ujumla.