Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka watoto wa Kitanzania kujiwekea malengo na kusoma kwa bidii ili kupata maarifa yatakayolisaidia taifa kupata maendeleo.

Amesema kuwa kwa upande wa Serikali itaendelea kuweka mazingira bora ya kujifunza na kufundishia ili kuwawezesha kufikia malengo hayo.

Amesema hayo leo Januari 24, 2022 mara baada ya kukagua ujenzi wa madarasa katika shule ya Sekondari Gehandu na Nowu zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara. Ujenzi wa madarasa hayo unatokana na fedha za Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO 19.

Ameongeza kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ameiagiza Wizara ya Elimu kufanya mapitio ya sera ili kuifanya sekta hiyo kuendelea kufanya vizuri zaidi

Pia Waziri Mkuu ameziagiza Halmashauri zote nchini kuweka mpango wa ujenzi wa mabweni kupitia mapato ya halmashauri na itakapotokea Serikali imeweka mpango wa ujenzi wa mabweni itatumika kama ujazilizi kwenye fedha hiyo

“Anzeni ma watoto wanaotembea umbali mrefu, hili linawezekana mkiweka mpango mzuri”

Aidha, Waziri Mkuu amewakumbusha watumishi wa umma kutambua kuwa wanajukumu kubwa la kuwatumikia watanzania na kutekeleza maelekezo ya ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi.

Pablo awapongeza wachezaji Simba SC
Wema huwa unajipambanua wenyewe