Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema serikali haitawavumilia watu wote wanaotumia vibaya fedha za umma ambazo zinapaswa kuleta maendeleo kwa wananchi zikiwemo fedha za mfuko wa Ukimwi.

Ameyasema hayo wakati akifungua kongamano la kitaifa la maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani, lililofanyika jijini Dar es Salaam. ambapo amesema kuwa serikali itawashughulikia wote wakiwemo wale wanaotumia vibaya fedha za Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi.

“Nitoe wito kwa Bodi ya Mfuko huu na watendaji wake kuhakikisha wanasimamia kikamilifu fedha hizi ili ziweze kufanikisha malengo ya kuanzishwa kwa Mfuko huu,” amesema Majaliwa

Aidha, mesema kuwa mfuko huo unalenga kufanikisha ukusanyaji wa fedha za kutosha ambazo ni muhimu wakati huu ambao taifa linaazimia kumaliza ukimwi ifikapo mwaka 2030.

Hata hivyo, Majaliwa amesisitiza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli itaendelea kutenga fedha za mfuko huo na kuhamasisha wananchi, wadau na sekta binafsi kuchangia mfuko huo muhimu

Picha: Kilimanjaro Stars yajiandaa na Challenge Cup 2017
Dr Nassoro Ally Matuzya afichua kinachomtesa Kamusoko