Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameipa wiki mbili Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), kuanzia Desemba 18, 2020 ihakikishe hadi Januari Mosi, 2021 bandari ya kimkakati ya Kagunga Mkoa wa kigoma wilayani Kigoma iwe imeanza kutoa huduma.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana Desemba 18 baada ya kukagua mradi wa bandari hiyo, iliyopo kwenye mwambao wa Ziwa Tanganyika wilayani Kigoma, ambapo alichukizwa na kitendo cha bandari hiyo kushindwa kutoa huduma licha ya kuwa imekamilika.

Mradi wa ujenzi wa bandari hiyo ulikamilika mwaka 2017 ukihusisha ujenzi wa jengo la abiria pamoja na mizigo, nyumba ya kuishi mtumishi na jengo maalumu lakini hakuna mtumishi katika bandari hiyo ambayo ujenzi wake uligharimu shilingi Bilioni 3.8.

Aidha, ameagiza kuletwa watumishi kwenye bandari hiyo ili waweze kufanya kazi na kuwatumikia wananchi.

Waziri Mkuu pia alishangazwa na kuchukizwa na kitendo cha meneja wa bandari kutoka makao makuu ya TPA kutokufika katika bandari hiyo tangu apangiwe na kwamba haijui.

Serikali yataifisha Almasi
Marekani yaidhinisha matumizi ya chanjo ya pili ya Covid 19