Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Kassim Majaliwa amepokea wanachama wapya 37 kutoka vyama vya CUF na CHADEMA ambao wameamua kurejea Chama cha Mapinduzi (CCM).

Kwa mujibu wa Katibu wa CCM wa wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi, Barnabas Essau amesema kuwa wanachama 35 kati ya hao wametoka CUF na wawili wametoka CHADEMA ambao wameamua kujiunga na chama cha mapinduzi huku wakisema wameridhishwa na utendaji kazi wa viongozi.

Essau amesema kuwa wanachama hao wote wametoka kata za Mbekenyela na Matambalale, hivyo wamekabidhiwa kadi mpya za CCM na kula kiapo cha uaminifu wa kukitumikia chama hicho.

Aidha, akizungumza kwa niaba ya wanachama wenzake wapya, Mohammed Issa Ndogoro ambaye amehamia kutoka CHADEMA, amesema kuwa wamejiunga na CCM baada ya kuridhishwa na mwelekeo wake, huku akisema kuwa wameguswa na jinsi Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli inavyofanya kazi ya kutatua kero za wananchi.

Hata hivyo, amesema kuwa amekaa upinzani kwa miaka 23 lakini anaikubali CCM sababu ya uwazi wake na ameshangaa kuona akipewa kadi na stakabadhi ya walipo yenye jina lake, jambo ambalo hajawahi kuliona katika vyama vingine vya upinzani.

 

 

Andrea Pirlo atundika daluga
Afukuzwa kazi kwa kuuonyesha kidole cha kati msafara wa Trump