Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewataka Viongozi wa Serikali kutumia fursa ya mafunzo wanayoyapata mara kwa mara kujiimarisha zaidi katika Uongozi na Utendaji kazi wao wa kila siku.

Ameyasema hayo Jijini Dodoma alipokua akifungua mafunzo ya siku Tano kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala Mikoa ya Tanzania bara yaliyoandaliwa na Taasisi ya Uongozi.

Amesema kuwa Rais na wasaidizi wake wana imani kubwa na uongozi na utendaji kazi wa viongozi hao na kwamba hawana shaka yeyote.

“Mada zilizochaguliwa ni muhimu na muafaka katika kuboresha Uongozi na Utendaji kazi hivyo kila mmoja wenu ajithathmini kupitia mafunzo haya kisha aboreshe zaidi utendaji kazi wake ili tuweze kumhudumia vizuri Mtanzania” Amesema Majaliwa.

Aidha, ameongeza kuwa katika mada inayohusu Majukumu na Mipaka ya kazi watajifunza namna ya kufanya kazi bila mikwaruzano isiyo na tija baina yao na viongozi wa mihimili mingine ya Dola, Viongozi wa Kisiasa na Watendaji wengine Serikalini.

Hata hivyo, amebainisha kuwa katika mada ya Uongozi, Hisia na Mahusiano Mahala pa kazi kuwa Viongozi hao watafahamishwa kwa undani mbinu za kuwaongoza watumishi walio chini yao kwa kujenga na kudumisha mshikamano na ushirikiano wa pamoja (Team work).

 

Modric avunja ufalme wa Messi na Ronald Ballon d'Or
Rais Trump, mkewe watoa heshima zao za mwisho kwa Bush