Serikali imetunga Sheria kali zinazowalinda watoto wa kike ambapo watakaobainika kuwapa ujauzito na kukatisha masomo yao adhabu watakayoipata hawatoisahau maisha.

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Mwakizega wilaya ya Uvinza akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Kigoma.

Amesema kuwa Serikali itatoa adhabu kali kwa mtu atakayebainika kukatisha elimu ya mtoto wa kike iwe kwa kumuoa au kumpa ujauzo.

Aidha, ameongeza kuwa watoto wa kike wanatakiwa kuheshimiwa katika jamii na waachwe waendelee na masomo yao kwani elimu ni haki yao ya msingi.

“Tukikukuta na mwanafuzni wa kike kwenye kona zisizoeleweka adhabu yake ni kifungo kisichopungua miaka 30 gerezani, hivyo vijana kuweni makini,” amesema Majaliwa.

Hata hivyo, Majaliwa amewataka wazazi na walezi kushirikiana na Serikali kuhakikisha watoto wa kike wanapelekwa shule na wanamaliza masomo yao.

 

Gianluigi Buffon aahidi kupambana PSG
JPM awakaribisha mabalozi jijini Dodoma