Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewataka wanafunzi wa kike wanaosoma shule mbalimbali nchini kusoma kwa bidii na wasikubali kushawishika.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Wasichana WAMA Sharaf iliyopo mkoani Lindi, ambapo amesema kuwa Serikali imeweka sheria kali kwa wote watakaobainika kukatisha masomo ya watoto wa kike kwa kuwapa ujauzito au kuwaozesha.

Aidha, Waziri Mkuu amewataka wanafunzi hao wa kike kuhakikisha wanatumia muda wao vizuri kwa kusoma kwa bidii na hatimaye watimize malengo yao.

“Nawasihi mtumie muda huu kusoma kwa bidii ili muweke msingi imara ya kujenga maisha yenu ya baadae. Msikubali kushawishika na kukatisha masomo yenu,”amesema Majaliwa

Amesema ni vema wanafunzi hao wakatumia vizuri fursa hiyo ya elimu wanayoipata shuleni hapo kwa kusoma kwa bidii na wafuate ratiba itakayokuwa inapangwa.

Naye, Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA, Mama Salma Kikwete ambaye pia ni mbunge wa Kuteuliwa alisema shule hiyo inasomesha watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu kutoka mikoa yote nchini.

Facebook kuonyesha ligi ya Uingereza?
Video: Itazame ngoma mpya ya Aslay 'Natamba'