Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameliagiza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kuwachukulia hatua kali wananchi wote wanaotumia vibaya namba za mawasiliano za jeshi hilo kwa kutoa taarifa za uongo kuhusu matukio ya majanga ya moto.

Ametoa agizo hilo wakati wa ziara katika Kituo cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura ya Maafa pamoja na Kituo cha Zimamoto na Uokoaji cha mkoa wa Ilala.

“Ili kudhibiti wananchi wanaopiga simu za kuomba msaada wa kutaka kuokolewa, huku kukiwa hakuna tukio lolote la janga la moto lililotokea kwenye maeneo yao, ni vyema watu hao wachukuliwe hatua kali ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo,”amesema Majaliwa

Ameyasema hayo mara baada ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,  Thobias Andengenye kumueleza baadhi ya changamoto zinazo likabili jeshi hilo kuwa ni pamoja na wananchi kupiga simu wakidai kuna ajali ya moto imetokea katika maeneo yao na baada watu wa uokoaji kufika wanabaini ni uongo.

Hata hivyo, Majaliwa amelitaka jeshi hilo kuwashawishi wakazi wa maeneo ya mabondeni kuondoka kabla ya kutokea kwa maafa badala ya kusubiri majanga yatokee, pia amewataka wawe na mpango wa kuonyesha eneo lenye maafa na kuujulisha umma.

 

Urusi 2018: Nani atabeba Kombe? Tuimulike Ubelgiji
Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Juni 9, 2018