Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka viongozi wanaoshiriki kozi fupi ya tano ya viongozi wahakikishe watakaporudi kwenye maeneo yao ya utendaji wawe wamebadilika kimtazamo, kihoja, kiushauri pamoja na utoaji maamuzi.
Ameyasema hayo wakati akifungua kozi ya tano ya muda mfupi ya viongozi inayofanyika katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi, Kunduchi jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa chuo hicho kilianzishwa kwa lengo la kulisaidia Taifa kujenga uwezo wa viongozi ili wanaohitimu mafunzo hayo wawe na uchambuzi wa kina na wa kimkakati ili kuweza kutatua mambo mbalimbali ya usalama wa Taifa na matatizo yanayotakiwa kushughulikiwa kimkakati.
“Chuo hiki kilianzishwa ili kuwaleta washiriki kutoka taasisi zote za Serikali na sekta binafsi waweze kujadili mambo mbalimbali ya kimkakati ili wanapokuwa wanatekeleza wajibu wao watambue kuwa ni kwa kiasi gani matokeo ya maamuzi yao yataathiri mambo ya kijamii, kiuchumi, uhusiano wa kidiplomasia na siasa za ndani kwa ujumla wake,”amesema Majaliwa
-
Dkt. Ashatu Kijaji ainyooshea kidole TBA
- Kamwelwe akazia ving’amuzi kufuata sheria, Clouds TV, ITV zaondolewa
-
Rais Magufuli afanya teuzi mpya zaidi ya nafasi 41
- Kwa upande wake Mkuu wa chuo hicho Luteni Jenerali, Paul amesema mafunzo hayo yanayoanza leo Agosti 13 yanatarajia kumalizika Agosti 17, ambapo mafunzo hayo yamelenga kuwanoa na kuwawezesha washiriki kujua mambo ya Usalama wa Taifa na uzalendo kwa nchi.