Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewataka Watanzania kuendelea kuliombea Taifa ili liendelee kudumu katika hali ya amani na utulivu.

Ameyasema hayo mapema hii leo mjini Dodoma wakati wa swala ya ijumaa katika msikiti Al-Gadaf, amesema kuwa suala la kudumisha amani na utulivu ni jukumu la kila mmoja, hivyo kila mwananchi kwa imani yake ahakikishe anashiriki kutunza hali hiyo.

“Tuendelee kudumisha amani, tufanye ibada kila mtu kwa imani yake. Serikali inaheshimu dini zote kwa sababu ndizo zinazojenga amani na mshikamano,” amesema Majaliwa.

Hata hivyo, Majaliwa amewataka wazazi wahakikishe wanawalea watoto wao katika mazingira ya kidini ili wanapokuwa watu wazima waje kuwa raia wema katika nchi yao hivyo kujenga moyo wa uzalendo.

 

Mbivu na mbichi kujulikana leo UEFA
Jukwaa la wazalendo latoa pongezi kwa Rais Dkt. Magufuli