Mjumbe wa kamati ya Halmashauri kuu Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na waziri mkuu ,Kassim Majaliwa amesema kuwa serikali inapanga kuanzisha mamalaka ya maji wilaya ya Chemba mkoani Dodoma .
Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni za chama hicho ,Majaliwa amesema kuwa kutokana na wilaya ya Chemba kutokuwa na mamlaka ya maji serikali itaanzisha mamlaka ya maji ili kuwezesha usimamizi wa upatikanaji wa maji wilayani humo.
“wilaya hii haina mamalaka ya maji . Kwa hiyo tutaanzisha mamlaka ya maji ili watumishi wawepo wilayani . wasimamie kwa karibu na waweze kufuatilia vyanzo vya maji kutokea hapa Chemba wakati tukiendelea kutatua tatizo la maji wilayani hapa tutaunda mamlaka ya maji hivi karibuni,” amesema Majaliwa .
Amesisitiza kuwa serikali ilishatoa pesa shilingi billion 1.6 kutafuta vyanzo vya maji katika vijiji vya Orada,Kisanga ,Moi ,Mondo na Ndaki wilayani humo kama ishara ya kuanza kwa utendaji .
Waziri mkuu Majaliwa anaednelea na mikutano ya kampeni za uchaguzi wilayani Kondoa Mkoani Dodoma.