Waziri  Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa leo pindi akifungua ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa amezungumzia mchakato mzima wa serikali kuhamia Dodoma na kusema Rais wa Jamuhuri  ya muungano wa Tanzania, John Pombe  Magufuli  kuhamia rasmi  mwakani.

“Leo nafungua ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa hapa Dodoma, zaidi ya watumishi 2376 wameshahamia Dodoma, mimi tayari nimehamia mapema, Makamu wa Rais Samia Suluhu ataungana nasi mwishoni mwa mwezi huu , mwakani tunategemea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli atahamia huku”, amesema Majaliwa.

Mpango huo wa kuhamia Dodoma ulianzishwa na aliyekuwa Baba wa Taifa  Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1973 na utekelezaji wake umeanza kufanyika rasmi mwaka 2017 ndani ya uongozi wa Rais John Pombe Magufuli.

Aidha Majaliwa amesema hadhi ya mkoa wa Dar es salaam haitopungua ila itakuwa sehemu rasmi ya biashara.

Hata hivyo amesema kuwa Viongozi kuhamia Dodoma hakuharibu hadhi ya mkoa huo, bali kunuufanya mkoa huo kubakia kuwa ni sehemu sahihi ya biashara kutokana na maendeleo makubwa yanayokuja kwani kutatengenezwa njia sita ambazo zitatoka Ubungo hadi  Chalinze, na kunaimarisha mwendokasi ili ufike katika maeneo kmengi.

Kilimanjaro Stars yaufyata kwa Z,bar Heroes
Mambosasa aifumua upya kesi ya Dk Shika