Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa amekagua barabara ya Mbamba Bay Njombe yenye kilometa 66 na kuzindua safari ya meli mpya MV Mbeya II katika Bandari ya Mbamba Bay wilayani Nyasa mkoani Ruvuma itakayotoa huduma ziwa Nyasa na nchi jirani za Msumbiji na Malawi.

Amesema kuwa ujenzi wa meli hiyo yenye thamani ya shilingi bilioni 9.1 ni mwendelezo wa serikali ya awamu ya Tano katika kuboresha miundombinu ya usafiri na usafirishaji wa mizigo na abiria kwa lengo la kuboresha uchumi.

Aidha Waziri amewahasa Vijana kuanza biashara kutoka nyasa kwenda Mbeya, Malawi na Msumbiji kwani serikali inaboresha miundombinu kwa maendeleo ya uchumi wa mtu mmoja mmoja.

Ameeleza kuwa serikali inajenga meli kubwa ya abiria na mizigo itakayokuwa inafanya shughuli zake eneo la ukanda wa bahari kwenda nchi jirani ikiwemonchi ya Comoro na maeneo mengine.

Aidha Serikali inajenga bandari kubwa ya karema kwa bilioni 47 pamoja na kuboresha ziwa victoria, pia Serikali inaendelea kujenga miradi ya usafiri na usafirishaji na kufungua fursa za kijiografia kila eneo.

Vikao vya CHADEMA kutaja iliko hatima ya Mdee na wenzake
Wanafunzi kusoma kwa zamu- Dar