Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia Watu watano ambao ni Issa Karim maarufu Mdaka Bomu (33) wa Mbezi, Mohamed Juma maarufu (Miaka 31) wa Mbezi Mwisho, Selemani Seif maarufu Dullah Kishandu (34) wa Mbezi Mwisho, Samsoni Joseph maarufu Mjeuri (32) wa Mbezi na Ezekiel Kennedy maarufu Simba MC wa Mbezi kwa tuhuma za mauaji.

Hayo yameelezwa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamilius Wambura ambapo amesema, Mei 8, 2021 majira ya mbili usiku Mikocheni A Watuhumiwa walivamia Bar iitwayo Imbizo na kumshambulia kwa mapanga na marungu Mlinzi (Regan Sylivester) na kusababisha kufariki dunia papo hapo.

Watuhumiwa hao wananatuhumiwa kuhusika na tukio la unyan’ganyi wa kutumia silaha huko Mabwepande May 07, 2021 saa tatu usiku ambapo walivamia Petrol station ya MEXONS na kuwashambulia Walinzi, Wahudumu na Wateja na kupora Tsh 2,440,000/= na kisha kupora silaha ya walinzi aina ya ‘short gun’

Kaiika tukio lingine, Wambura ameeleza kuwa Machi 18, 2021 saa mbili usiku majambazi watano walivamia nyumbani kwa Mkurugenzi wa Benki ya Azania Mbweni Mpiji Dar es salaam na kuwashambulia Walinzi wa kampuni ya SUMA JKT na kuwapora silaha aina ya short gun pump action ikiwa na risasi tano.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum DSM lilifanya ufuatiliaji na kufanikiwa kukamata silaha hiyo Mei 20, 2021 pamoja na Watuhumiwa watano waliohusika katika tukio hilo.

Aidha, jeshi hilo linawashikilia watuhumiwa wanne ambao ni Babuelly Simon Chao (43) Mkazi wa Moshi, Sebastiani Shembaru (36) wa Kigamboni, Hussen Misanya (33) wa Mabibo Relini na Said Rajabu (16) wa Mabibo, wanaotuhumiwa kuiba magari maeneo ya Kinondoni na Ilala na walikamatwa na magari manne ambayo ni T 817 ATQ Toyota Nadia, T 134 BPJ Toyota IST, T 952 CKB Toyota Mark II Grand 4 na T 590 DTK Toyota IST.

Mbali na magari hayo, Polisi pia wamekamata Pikipiki (MC 136 CSA Boxer) iliyoibiwa Mei 15, 2021 Kibamba shule na kupelekwa Gairo, Morogoro. 

Bodi ya mikopo kufuta tozo kwa wanufaika
KMC FC waitwa kambini FASTA