Majambazi wamelipua lango la benki tano na kupora katika benki hizo, katikati ya mji wa Offa nchini Nigeria katika tukio la ujambazi lililodumu kwa takribani saa moja na kusababisha vifo vya polisi sita pamoja na raia sita.
Msemaji wa jeshi la polisi jimbo la Kwara, Ajayi Okasanmi ameviambia vyombo vya habari kuwa jeshi hilo limeanza uchunguzi na linawahoji mameneja wa mabenki husika, pamoja na mambo mengine kufahamu ni kiasi gani cha fedha zilizoporwa na majambazi hao.
Majambazi hao waliokuwa na silaha nzito walianza kwa kushambulia kituo cha polisi cha Owode ambapo waliwaua askari na baadaye kuvamia mabenki hayo yaliyoko katikati ya eneo la soko.
Jeshi la polisi lilifanikiwa kuyapata magari yaliporwa na majambazi hao wakati wa tukio hilo, kwa mujibu wa Okasanmi.
- Zimbabwe yapiga marufuku ‘mahubiri ya mafanikio’ kwenye TV, redio
- Kaya 45 zaathirika na mvua mkoani Kagera
Alieleza kuwa polisi walishindwa kuwadhibiti majambazi hao kwakuwa walikuwa wakifyatua risasi kimkakati katika eneo ambalo lina watu wengi, hivyo ilikuwa hatari kufanya majibishano.
Jeshi la Polisi limeahidi kufanya msako mkali kuwabaini na kuwakamata waliohusika na tukio hili.