Watu wanaoaminika kuwa ni majambazi wamevamia kituo cha polisi cha Stakishari, Ukongo, Dar es Salaam wakiwa na silaha za moto na kufanya mauaji ya kutisha usiku wa kuamkia leo.

Taarifa kutoka kwa mashuhuda zimeeleza kuwa miongoni mwa watu saba waliouwawa na majambazi hao ni askari wanne, mgambo mmoja na raia wawili. Mmoja kati ya majambazi hao pia aliuwawa.

Watu mbalimbali wametumia mitandao ya kijamii kupost picha za madhara ya tukio hilo huku baadhi ya wakazi wa maeneo hayo wakitoa pole kwa ndugu na jamaa za waliopoteza maisha.

Jeshi la polisi bado halijatoa taarifa rasmi kuhusu tukio hilo.

Sterling Ashinda Vita, Liverpool Wakubali Kumuachia
Dr. Slaa Abeza Nguvu Ya Magufuli Dhidi Ya Ukawa, ‘Hatuwezi’