Waziri wa Nishati, January Makamba amesema ndani ya msimu mmoja wiki iliyopita Wizara ya Nishati imefanikiwa kujaza maji kwa kiwango kinachotosheleza kuzalisha umeme kwenye Bwawa la Julius Nyerere.

Pia, kina Cha bwawa lote lile ni mita 184 kutoka usawa wa Bahari, kina kinachotakiwa kufikiwa ili uanze kuzalisha umeme ni mita 163 kutoka usawa wa Bahari na siku ya Jana imefikia mita 163.61.

Waziri Makamba ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam na kusema hadi sasa mradi wa kufua umeme Rufiji Julius Nyerere unaendelea kwa Kasi kubwa na sasahivi ambapo umefikia asilimia 89 na hadi kufikia mwezi Julai mradi huo utafikia asilimia 90.

”Huko nyuma kumekuwa na hofu kubwa ya je maji yatajaa kuweza kuzalisha umeme katika bwawa hilo, tulikadiria tutakuwa na misimu mitatu ambayo ndiyo itatosheleza kujaza bwawa hilo lakini ndani ya msimu mmoja wiki iliyopita Wizara ya Nishati imefanikiwa kujaza maji kwa kiwango kinachotosheleza kuzalisha umeme kwenye bwawa la Julius Nyerere,” alisema.

Aidha Makamba amebainisha kuwa kazi ya ufungaji mitambo inaendelea na mnamo mwezi wa pili wataanza kufanya majaribio ya kuzungusha mitambo kwa maji. >> “Imani yetu ni kwamba mwezi wa 6 mwakani tutaanza kutoa umeme pale Julius Nyerere na kuingiza umeme wa kwanza kwenye gridi ya Taifa” – Waziri Makamba.

Kuhusu Ujazo wa bwawa la Julius Nyerere, Makamba amesema ni mita za ujazo Bilioni 30 Hadi kufikia Juzi (July 04 2023) maji yaliyoingia ndani ya Bwawa ni mita za ujazo Bilioni 13.8 ambao ni sawa na asilimia 43.

Simon Msuva: Kibabage ana kazi kubwa Young Africans
Wakufunzi DPA washindi Mpira wa Pete Polisi Jamii Cup