Mapigano yameendelea kuripotiwa katika baadhi ya maeneo ya mji mkuu wa Sudan Khartoum, kati ya wanajeshi wa serikali na wapiganaji wa RSF wakati huu ambapo mzozo baina ya pande hizo mbili ukiwa unaendelea.
Katika taarifa yake iliyochapishwa kwenye ukurasa wa Facebook, Jeshi limethibitisha kuzuia shambulio lengine na wapiganaji wa RSF kwenye kambi yake katika iliyopo eneo la Al-Shajara, kusini mwa Khartoum.
Kwa upande wao, wapiganaji wa RSF kupitia ukurasa wa X zamani ukijulikana kama twitter, walidai kuchukua udhibiti wa baadhi ya maeneo katika kambi hiyo pamoja na kuchukua silaha za kijeshi.
Televisheni ya AI Arabiya inayofadhiliwa na Serikali ya Saudi katika mtandao wake iliripoti kuwa Jeshi la Sudan bado linadhibiti kambi hiyo, baada ya siku tatu za mapigano makali.