Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi ameagiza tume ya ya uchunguzi wa majengo ya kihistoria yaliyopo katika Mji Mkongwe atayoiunda, kuwahihi kutoa orodha ya majengo chakavu yanayopaswa kufungwa ili kuepusha ajali.
Akizungumza leo Disemba 28, 2020 alipokutana na wadau wa mji huo, amesema hatua hiyo itasaidia kuthibibiti maafa kama yaliyotokea katika jumba la maajabu la Beit Al Ajaib lililoporomoka na kufukia watu takribani watatu siku ya sikuku ya krismass.
Rais Mwinyi ameagiza tume hiyo atakayoiunda hivi karibuni kubaini wananchi walioko karibu nayo ili waamishwe haraka kabla hawajakumbwa na maafa.
”Ni vizuri hivi sasa tubainishe wazi kwamba majengo gani yanafaa yafungwe yafungw mara moja kabla hajasababisha ajali, ni vizuri tuhakikishe wakazi gani amabo wako pale wanapaswa kuhamishwa mara moja kabla hayajatokea maafa” amesema Rais Mwinyi
Hata hivyo amesema kuwa serikali yake itatenga bajeti ya fedha pamoja an kuunda mfuko maalumu wa ujenzi wa Mji Mkongwe na kuomba wadau mbalimbali kutoa mchango wao wa kifedha ili kuuhifadhi mji huo wa kihistoria.