Majengo yanayotumiwa na tume ya taifa ya uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yameteketea kwa  moto jijini Kinshasa.

Inasemekana kuwa moto huo ulizuka mishale ya saa nane usiku na kuzua taharuki ikizingatiwa kwamba ni siku 10 tu zilizobaki kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini humo.

Moto huo unadaiwa kuathiri majengo ambayo yamekuwa yakitumiwa kuhifadhi nyaraka na vifaa vyote vinavyo tarajiwa kutumika katika uchaguzi huo, ambapo chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.

Aidha, Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi hiyo, Henri Mova Sakanyi amesema kuwa uharibifu uliotokea ni mkubwa, ambapo inasemekana kuwa kulikuwa na mashine takriban 7,000 za kupigia kura ambazo zimeharibiwa.

“Ni matumaini yetu kwamba tukio hili halitvuruga mchakato mzima wa uchaguzi, kwasasa uchunguzi unaendelea ii kuweza kubaini chanzo cha moto huu,” amesema Jean Pierre Kalamba, msemaji wa tume ya uchaguzi (CENI)

Hata hivyo, kampeni za uchaguzi huo zimekumbwa na ghasia katika baadhi ya maeneo nchini humo,

 

 

Machali awatupia zigo wanahabari 'Siku hizi hawafuatilii kazi zangu'
Afrika yaongoza kwa rasilimali ya maji baridi