Wanajeshi watano wa DR Congo wameuawa na wanajeshi wa Rwanda baada ya kutokea mapigano makali katika mpaka wa nchi hizo.
Jenerali Bruno Mandevu amesema kuwa mapigano hayo yalizuka katika mbuga ya wanyama ya Viunga vya ardhi ya Congo, ambapo Rwanda imekana kuhusika katika mapigano hayo.
Amesema kuwa wanajeshi wa Congo walidhania kuwa walikuwa wakishambuliana na waasi waliopo katika eneo hilo kumbe walikuwa ni wanajeshi kutoka Rwanda.
Aidha, Msemaji wa jeshi la Rwanda Kanali, Innocent Munyengango amethibitisha kutokea kwa mashambuliano hayo na kusema kuwa hakukuwa na majeruhi upande wa Rwanda.
”Jeshi la Congoleese lilivamia kambi yetu na kutushambulia. Wanajeshi wetu walilazimika kujitetea kwa kujibu mashambulizi hayo,”amesema Kanali Munyengango
Hata hivyo, Mashariki mwa taifa la DR Congo karibu na mpaka na Rwanda kumekuwepo na mapigano ya mara kwa mara kutoka kwa waasi na jeshi la nchi hiyo.