Halmashauri ya Jiji la Dodoma na Arusha zimeibuka vinara katika ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa robo ya kwanza ya mwaka wa Fedha 2018/19.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa. Selemani Jafo wakati wa kutoa taarifa ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa Fedha 2018/19.

Jafo amesema kuwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma imeongoza kwa kukusanya mapato ghafi yaani Fedha nyingi kuliko Halmashauri zote nchini, Jiji hilo limefanikiwa kukusanya kiasi cha Tsh. Bil. 14.4 kati ya bajeti yao ya kukusanya Tsh. Bil 68.6. makusanyo hayo ni sawa na aslimia 21 ya  malengo waliyojiwekea.

Wakati huo huo Arusha inaongoza kwa kukusanyanya vizuri kiasilimia na imefanikiwa kukusanya mapatyo kwa asilimia 26 ya malengo waliyojiwekea, hii ni kwamba Jiji la Arusha limekusanya kiasi cha Tsh Bil. 4.1 kati ya Tsh Bil.15.6 ya malengo yao ya makusanyo kwa mwaka wa Fedha 2018/19.

“Ieleweke wazi kuwa Jiji la Arusha ndio lililofanya vizuri kimakusanyo kwa mujibu wa asilimia lakini Jiji la Dodoma ndio lililokusanya Fedha nyingi zaidi kuliko halmashauri zote Tanzania,”amesema Jafo

Aliongeza kuwa kwa upande wa Halmashauri za Manispaa iliyofanya vizuri zaidi ni Manispaa ya Musoma na kwa Halmashauri za Mji zimeongozwa na Mbinga na upande wa Halmashauri za Wilaya zimeongozwa na Kisarawe.

Hata hivyo, ameongeza kuwa kwa makusanyo hayo ukiyaweka Kimkoa inaongozwa na Mkoa wa Simiyu ikifuatiwa na Manyara, kisha Lindi, Mara, Pwani, Arusha, Njombe,Dodoma, Mwanza na kumalizia na Geita.

 

20 mbaroni kwa kumteka mwanamke Muitaliano
Mkurugenzi ataja waliozimia Fiesta ‘ilipotesti mitambo’ Leaders