Hali ya hewa ya kisiasa mjini Dodoma imeanza kuutoa ukungu uliotanda miongoni mwa makada wa CCM wanaowania nafasi ya kugombea nafasi ya urais, masaa machache baada kufanyika kikao kizito cha Kamati ya Usalama na Maadili kilichoongozwa na mwenyekiti wa chama hicho,Rais Jakaya Kikwete.

Kikao hicho kinatarajiwa kuwa pamoja na mambo mengine kiliyapata majina ya wagombea watano yatakayowasilishwa kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa cha CCM (NEC) leo kwa ajili ya kuchagua majina matatu ambayo baadae yatawasilishwa mbele ya Mkutano Mkuu wa Taifa utakaofanyika Kesho.

Kikao hicho cha maadili kilichofanyika jana jioni baada ya rais kikwete kulihutubia bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kiliyapitia na kujadili majina ya wagombea 38, na kwa mujibu wa taratibu za chama hicho, kikao hichokinaweza kuwaalika pia viongozi wa vyombo vya usalama ili kupata taarifa za kina za kiusalama kabla ya kufanya maamuzi.

Akilihutubia bunge la Jamhuri ya Tanzania, Rais Kikwete aliwasihi wagombea ambao hawatafanikiwa kuchaguliwa na chama hicho wasinune kwa kuwa wako wengi kwenye mchakato huo unaolenga kumpata mtu mmoja.

“Nawatakia heri wagombea urais walioko humu na nawashukuru kwa kuonyesha nia ya kunipokea mzigo huu mzito. Mko wengi kweli, tena vigogo na safari hii tuna kazi kweli kuwapunguza hadi tubakize watano, lakini msininunie,”alisema Rais Kikwete.

Wakati mchakato huo unaendelea, vuguvugu linaendelea pia nje ya vikao hivyo ambapo watu na makundi mbalimbali wameanza kuyataja majina ya baadhi ya wagombea watano wanaopewa nafasi kubwa zaidi ya kuchaguliwa na Kamati Kuu.

Kada aelezea kuvuja kwa ‘Mkakati wa Kumuengua Lowasa’
Iker Casillas Afunguliwa Milango Ya Kuondoka Hispania