Serikali kupitia wizara ya fedha imeidhinisha jumla ya sh bilioni 43.39 kwa ajili ya kuwalipa watumishi 27,389 waliokuwa wakiidai Serikali na wametoa majina ya wafanyakazi wanaotakiwa kulipwa malimbikizi ya mishahara yao ambayo yana zaidi ya miaka kumi.
Waziri wa fedha na mipango, Dk Philip Mpango, amesema malipo hayo yameidhinishwa baada ya uhakiki wa watumishi 82,111 waliokuwa wakiidai Serikali.
Akitoa mchanganuo huo wa jinsi madeni hayo yatakavyolipwa, amesema fedha hizo zitajumuisha sh bilioni 16.25 kwa walimu 15.919 na sh bilioni 27.15 kwa watumishi wasiokuwa walimu.
Mpango amesema Serikali imeokoa jumla ya sh bilioni 84.22 kutokana na uhakiki huo ikiwemo kuwaondoa katika mfumo wa malipo ya mshahara watumishi hewa wenye vyeti feki na wasio na sifa.
-
WANAOSTAHILI KULIPWA MADAI
-
Nape ang’ata na kupuliza usalama wa taifa
-
Miguna adai atamng’oa Kenyatta madarakani
Pia amesema hadi kufikia julai mosi, mwaka jana Serikali ilikuwa na madai ya malimbukizi ya mishahara yenye jumla ya sh. 127,605,128,872.81
”Kupitia mfumo wa taarifa za utumishi na mishahara (HCMIS) Serikali ilikuwa inadaiwa kiasi hicho cha fedha hadi kufikia julai mosi mwak ajana. Madeni hayo yalikuwa kwa watumishi 82,111 wakiwamo walimu 53,925 waliokuwa wakiidai Serikali shilingi 53,940,514,677.23”amesema Mpango.