Chama cha waigizaji Tanzania, TDFAA kimekanusha taarifa iliyozuka na kusambazwa katika mitandao ya kijamii ikidai muigizaji wa vichekesho maarufu hapa nchini, Amri Athuman maarufu kama Mzee Majuto amefariki dunia.
TFDAA imesikitishwa sana na taarifa hiyo na kusema kuwa sio kweli kwani Mzee Majuto yupo hai na yupo nyumbani kwakwe mara baada ya kurejea nchini India alikokuwa akifanyiwa matibabu ya Ugonjwa wa tezi dume uliokuwa ukimsumbua kwa muda mrefu.
Aidha Chama hicho kimetoa onyo kali kwa wale wote wanaozusha na kusambaza habari hizo na kuomba zipuuzwe, kwa atakayekiuka agizo hilo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Taarifa hiyo imetolewa Leo, Juni 26, 2018 na Afisa habari wa Chama cha Waigizaji Tanzania, M. Kaftany.
Hata hivyo hii ni mara ya pili kwa Mzee Majuto kuzushiwa taarifa hiyo mbaya.