Maandamano ya kupinga ukali wa maisha nchini Kenya, yameacha simanzi kufuatia ripoti ya vifo vya Watu sita vilivyotokea katika miji ya Mlolongo na Kitengela nje kidogo ya mji mkuu wa Nairobi ikisadikika waliuawa katika mapambano kati ya Polisi na waandamanaji.

Baada ya ghasia hizo za Jumatano Julai 12, 2023 Waziri wa Mambo ya Ndani nchini humo, Kithure Kindiki alitoa onyo akisema Serikali haitavumilia tena, kauli ambayo inarandana na ile aliyoitoa Rais William Ruto.

Kithure alisema, “Watu wamepoteza maisha, maafisa kadhaa wa usalama na raia wamejeruhiwa vibaya na hasara kubwa kwa uchumi wa nchi imetokea, ghasia zilizotokea katika maeneo kadhaa zimesababisha uporaji na uharibifu wa mali za watu binafsi na umma.”

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga, anaendeleza kampeni ya kuipinga Serikali, na aliitisha maandamano ya kupinga sheria ya fedha 2023 ambayo imesababisha bei ya mafuta kupanda, na kuongeza ukali wa maisha kwa  Wakenya.

Azam FC kukipiga na Al Hilal Omdurman
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Julai 13, 2023